We Accept: Pay by Mpesa Pay by Tigo Pesa / Airtel Money Pay by CRDB Bank Transfer or Deposit DPO

Historia, Muundo na Faida kuu 5 za kutumia .tz kwa biashara au taasisi yako

Moja kati ya ya maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu matumizi ya majina ya website (domain names) ni je kuna tofauti yoyote kati ya domain za .tz na zile za .com? Pia, wengi wamekuwa na hofu kubwa juu ya ubora na upatikanaji wa kikoa cha .tz pindi wanapoanza kutumia wakihofia kuwa ipo siku domain inaweza isipatikane kutokana na uwezo wa kitaalamu au sababu nyingine. Watu wengi wamekuwa na hisia tofauti tofauti na wengine hata kuanza kuhisi kuwa labda website zao zitaweza kufungiwa kiurahisi na mamlaka kama watatumia majina ya .tz.  Maswali haya ni sehemu ya yale ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza bila majibu ya moja kwa moja. Duhosting tukiwa ni moja ya Wasajili wakubwa wa kikoa cha .tz tuliosaliwa na mamlaka wa mawasiliano ( .tz domain registrars), tutakujuza jinsi gani domain inafanya kazi, historia yake, faida za kutumia .tz. 

 

Utofauti kati ya Jina la website (Domain name) na Website

Moja ya vitu ambavyo watu wengi wamekuwa wakichanganya ni kuwa, website na Domain wakichukulia ni kitu kimoja. Hivi ni vitu viwili vinavyofanya kazi kwa kushirikiana. Website ni muunganiko wa kurasa za kwenye mtandao zinazotambulishwa kwa kutumia jina moja (Domain Name) zikiwa zimehifadhiwa na kuchapishwa (Published) angalau kwenye server moja inayopatikana katika mtandao wa Internet. Wakati Domain name ni jina linaloitambulisha website kwenye ulimwengu wa mtandao (Internet), mfano dulaw.co.tz ni domain name lakini ndani yake kuna system kwa ajili ya kurahisisha kazi za wanasheria. Hivyo unaweza kuwa na website bila jina na pia unaweza kuwa na jina bila Website lakini hakuna kimoja kinachoweza kufanya kazi bila ya mwingine (Vinashirikiana). Pia, tunapozungumzia Website tunamaanisha ni sehemu mojawapo ya aina ya taarifa zilizohifadhiwa kwenye mtandao lakini inaweza kuwa ni Software mfano Dulaw.co.tz , Application mfano TanzMED, Email, Kifaa cha kwenye mtandao (IOT) nk. Zote hizi zinatumia domain kuweza kufikia mafaili au kifaa husika. Kwa lugha rahisi, Domain ni utambulisho/ jina wa kifaa au website kwenye mtandao, badala ya kuita Kibabla kwenye mtandao utaita duhosting.co.tz. Hivyo unaweza kununua jina la Website sehemu nyingine na ukafanya Web Hosting sehemu nyingine kabisa.

 

Historia ya majina ya Website (Domain Names):

Vifaa vilivyopo kwenye mtandao, kama website, App nk hutumia anuani za mtandao  (IP Address) kuwasiliana, sawasawa na hizi anuani za makazi na namba za nyumba zinazobandikwa hapa Tanzania kwa sasa. Mfano, kama unataka kuifungua website ya Duhosting unaweza pia kuipata kupitia http://198.207.55.196. Ngoja kidogo, je unaweza kuzikariri hizi namba? Hii n diyo sababu ikapelekea kugunduliwa kwa majina ya Webite ili kuwa mbadala wa IP. Mnamo mwaka 1984 wataalamu wa Chuo kikuu cha Wisconsin walitengeneza mfumo unaowezesha kuhusianisha majina ya website pamoja na anuani zao (IP Address) na kuweka taarifa hizi kwenye server waliyoipa jina la DNS Server. Server hii huhifadhi taarifa zote za domains na kuhakikisha DNS server zote za duniani zina taarifa ya upatikanaji wake. Hivyo wakati unafungua Website yoyote, mawasiliano hufanyika kati ya server iliyopo na DNS server kutoa taarifa. Kumbuka, kuna DNS server nyingi sana duniani na zote huwa na taaifa zinazofanana, hii hupelekea hata kama moja itakuwa haipatikaniki, basi haitofanya Website iwe  haipatikani. 

Kulingana na taarifa zilizopo, ni kuanzia mwaka 1985 ambapo majina ya Website kwa kutumia vikoa vya .com, .net na .org yalianza kutumika na watu kuanza kuachana na namba.

Ujio wa .tz Domain

Baada ya miaka hiyo ya 1985 ambapo Domain names zimekuwa zikitumika duniani kote na biashara nyingi zimekuwa zikitumika, na watu wengi wamekuwa wakiendelea kunufaika na matumizi ya domain na kupelekea kuwa nyingi zaidi na zaidi. Kila miaka ilivyozidi kwenda ndipo kukaanza kuonekana umuhimu wa kuwa na domain zenye mipaka ya nchi (Country Code Domains au kwa kifupi ccTLD) na nchi nyingi zikaanza kuzikimbilia kutokana na faida nyingi zinazokuja nazo. Domain hizi ni kama .co.jp kwa Japani, .co.uk kwa Uingereza, .co.za kwa Afrika ya  Kusini au .co.ke kwa kenya. Kwa sasa, nchi zote duniani zinapendelea domain zenye vikoa vya nchi zake. Moja ya changamoto iliyopelekea nchi nyingi kukimbilia domain hizi za nchi ni kujaa kwa domain za .com mfano leo hii unataka kutafuta domain ya dulaw.com ni dhahiri kuwa hautoweza kuipata kwaku wenzetu wameshakuwa kwenye ulimwengu wa technlojia kwa miaka, ila ukitaka domain ya Dulaw.co.tz utaenda Duhosting na kuisajili. Kwa Tanzania, mchakato wa kuwa na doman za nchi ulianza mwaka 1995 na hatimaye mwaka 2006 kampuni isiyo ya faida Tanzania Network Information Center ilianzishwa kati ya TCRA (regulator) and TISPA (the association of ISPs) kwa lengo la kuratibu shughuli za domain na baadae kazi hiyo ikahamishiwa TCRA.

 

Mfumo wa Usajili wa Domain

Katika usajili wa domain kuna muundo rasmi katika ufanikishaji wa usajili, kila muhusika anakuwa na jukumu lake na ukomo wa majukumu kama ifuatavyo.

1. Mtunza taariza (Registry) (kwa .tz huyu ni TCRA ambaye anamiliki server zenye anuani za domain zote (DNS Server) lakini yeye hajihusishi na usajili wa domain moja kwa moja, hivyo hauwezi kwenda TCRA ukasajili domain. TCRA pia huweka miongozi ya namba ya usajili, kutambua wasajili na kupanga bei elekezi kulinga na mujibu wa sheria. Kwa Domain za .com kazi hii hufanywa na IANA.

2. Msajili (Registrar) (mfano Duhosting, Zesha, Killihost nk kama unavyoweza kupata orodha kamili ya wasajili kwenye Wavuti rasmi ya TCRA) Huyu ndiye kiungo kati ya mmiliki wa Domain (registrar) na mtunza taarifa za domain (Registry). Kazi ya registrar ni kuwa na mfumo unaomuwezesha mteja kufikia server za registry na kusajili, kuhuisha, kuhsamisha taarifa za  domain (name server) au kuhuisha taarifa za umiliki wa domain. Hivyo kwa sehemu kubwa, kazi hufanywa na registrar. registrars hupata kipato kutokana na commission inayopatikana kwenye zoezi la usajili kama ilivyoanishwa kwenye sheria.

3. Mmiliki (Registrants): Huyu ndiye mmiliki wa domain, yeye anahusika kwenye matumizi yote ya domain na chochote kinachotokea kwenye domain yeye ndiye muhusika mkuu. Lakini, kuna wakati kutokana na mfumo wa biashara wamiliki huamua kutumia mtu wa kati ili kukamilisha zoezi la usajili wa domain (Domain Resellers) ambao nao hupata gawio kutoka kwa Registrars au huweka kiasi fulani cha ziada kwa mteja kwa kila domain inayosajiliwa. lakini, mmiliki wa domain anatakiwa awe ni mtumiaji na siyo Reseller.

Mchoro unaonesha Muundo wa Domain

Faida za kutumia .tz domain

Hadi sasa, utakuwa umeshajua Domain ni nini, inafanya vipi kazi na muundo wake. Hivyo ni dhahiri ungependa kujua faida zaidi za kwanini unahitaji kumiliki domain ya .tz, makala hii itasaidia kujibu maswali yanayoweza kujitokeza kuhusu .tz domain.

1. Kupata jina unalolipenda (branding) na kuongeza uaminifu wa wateja

Kwakuwa .com imeshakuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu, majina mengi yameshachukuliwa, hivyo watu wengi wamekuwa wakihitajika kuweka neno tz mbele mfano kilitz.com badala ya kili.tz. Kwa kutumia .tz unaweza kuwa na jina jepesi na lenye mvuto kama marathon.tz . Hii ni ngumu sana kupatikana kwenye domain ya com. Hivyo kuwezesha wateja wako waikumbuke brand yako kiurahisi na hata kuweza kuwashirikisha wengine.

Pia, kwa kutumia jina la .tz huleta imani kubwa kwa wateja, hii inajionesha sana kwa taasisi au makampuni yanayofanya kazi na mataifa ya nje. Mfano NGO, asasi za kiraia, makapuni ya safari nk. Punde tuu mtumiaji anapoona .tz basi anakuwa na uhakika zaidi kwakuwa utaratibu wa usajili wa .tz umerasimishwa zaidi na ni ngumu sana kupata matapeli wa kwenye mtandao(Scam) wanaotumia domain za .tz.

2. Matokeo chanya kwenye mitandao ya taarifa (Search Engine Optimization)

Kulingana na tafiti ya mtandao wa Hotspot, 46%  ya matokeo ya utafutaji wa kwenye mtandao, Google Search hutafuta taarifa zilizo kwenye eneo la mtafutaji taarifa (local information). Kuna mambo mengi huchangia kujua kama taarifa hii ipo eneo lako au la. Pia, aina ya taarifa, jina la website na mambo mengine mengi huchangia kwenye hili. Mfano, leo hii ukienda kutafuta Website Hosting Companies in Tanzania kwenye Google ukiwa Tanzania, utaipata Duhosting moja kati ya makampuni ya juu kabisa. Hii ni kutokana na kuiboresha webste yetu kwa ajili ya soko la Tanzania.

 3. Urahisi wa utatuzi wa Migogoro ya Domain na hata kurudisha domain iliyopotea au kuibiwa

Tukiwa kama moja ya makampuni makubwa kwenye eneo la usajili wa Domain, moja kati ya kesi nyingi zinazotufikia ni wafanyabiashara / wamiliki wengi kutapeliwa domain zao na watu waliowaamini kuwasajilia. Mara nyingi waajiri huwaagiza wafanyakazi kusajili domain, sasa baada ya kuacha kazi au kutokuwa na maelewano mazuri hutumia domain kama fimbo katika kuhakikisha muajiri anafanya anachotaka mfanyakazi wakati domain ni mali ya muajiri. Pia, kuna wengine hupoteza mawasiliano na aliyewasajilia (Reseller). Kwakuwa usimamizi wa .tz unafanyika Tanzania moja kwa moja, hivyo, endapo kutatokea tatizo lolote na mtu aliyekusajilia domain ukashindwa kuwa na mawasiliano naye, basi ni rahisi kuwasiliana na Registrar na yeye atakuongoza katika taratibu za kisheria za kurudisha jina lako na hatimaye kutoathiri biashara yako. Na hata pale panapokuwa na mgogoro, TCRA huweza kumsaidia mmiliki wa biashara. Kuna watu wengi sana wamefaidika na hili na watakuwa mashuhuda.

4. Kurudisha Domain iliyofutwa bila malipo ya ziada wala kuchafua brand yako

Mara nyingi kwa domain za .com zinapofutwa, kuna watu online wametengeneza software (BOT) zinazofanya usajili mpya wa domain hiyo tena kwa kasi ya ajabu ambayo wewe kama binadamu hauwezi kushindana nayo, haswa zile zilizokuwa na watumiaji wengi kwa lengo la kuja kukuuzia tena kama utaitaka. Na wengine huzisajili kwa lengo la kuweka taarifa chafu kama picha za ngono, matangazo ya bet nk. Mfano mzuri kwa hapa Tanzania, ni jina la domain la mshauri Nasaa mmoja maarufu sana hapa nchini, leo hii ukitembelea domain yake, kumewekwa picha na video chafu zisizo na maadili. Kumbuka watu walikuwa wameshaizoea hiyo Website yake, sasa leo anafungua anaonana na mambo ya ajabu. Kimsingi wateja wataona hawapo salama tena na inaweza kupelekea kupoteza biashara. Kama umechelewa kulipia domain ya .tz ni ngumu sana kuona mtu ameichukua na pia kwa baadhi ya makampuni kama DuHosting tutakupigia simu na hata kukutumia sms kukukumbusha juu ya kuisha kwake.

5. Kutangaza nchi na kuongeza pato la taifa kwa kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni

Ndiyo, kwa kutumia vikoa vya .tz, tunasaidia kutangaza nchi yetu, na pia kuongeza mapato ya ndani kwakuwa hadi sasa hakuna msajili (registrar) wa .com hata mmoja kutoka Tanzania na kuna makampuni si zaidi ya 7 kutoka Afrika nzima yaliyosajiliwa na IANA. Hivyo kwa kutumia .com ina maana tunahamisha hela kwenda nje. Ikimbukwe kwamba watu wanapoona domain za .tz inawasaidia kuikumbuka Tanzania (Identity). 

 Je unahitaji domain ya .com?

Jibu la swali hili ni NDIYO au HAPANA, .tz ndiyo mpango mzima. Haijalishi unafanya biashara Tanzania pekee au dunia nzima, .tz itakufikisha huko na inatosha kabisa. Kumbuka, haijalishi unatumia kikoa cha .tz au .com, zote zitapatikanika dunia nzima. Tofauti tu, kwa kutumia .tz registry wake ni TCRA wakati .com ni IANA. kwa wale ambao wana domain za .org au .com wanaweza kuweka mpango wa kuhamia .tz bila kupoteza nafasi yako kwenye Google (Ranking) na wale wanaoanza unashauriwa kwenda .tz moja kwa moja kwakuwa kuna faida nyingi sana. Hata kama biashara yako inafanya kazi kwenye nchi nyingi, pia, unaweza kusajili domain kwa kila nchi na ukafungua kulingana na nchi husika, mfano ukiwa tanzania na ukafungua Google utapelekwa Google.co.tz

Kuna uoga au dhana ambayo ipo kwa watu wengi wetu ya kuhofia matumizi ya .tz ya kuamini kama .com ndiyo inayojulikana na watu au huko online hawaijui .tz, hii ni imani ya zamani sana. Internet imebadilika sana sasa na kuna maboresho makubwa kwenye mfumo wa utafutaji taarifa.

Unayo kila sababu ya kusajili .tz domain, gharama yake pia ni rahisi, huanzia elfu 12,000 hadi 25000 kwa majina ya kawaida ambapo .com huanzia 35,000 na kuendelea. Pia kwa sasa kuna majina ya premium ya .tz ambayo hayana .co mfano duhosting.tz kama tulivyoelezea hapa .

Upo tayari?   sajili Domain yako Hapa.